Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Happy amtupia dongo Faiza Ally

Ndoa Suguuu(1) Happy amtupia dongo Faiza Ally

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa legendary wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Mbili maarufu kama Sugu aitwaye Happy ametundika picha inayomwonesha akiwa na mumewe huyo kisha kuandika ujumbe unaodaiwa kuwa dongo kwa Faiza Ally.

"Siku ya mahari yangu!❤️ Hapo nishatoka kupewa mabunda yangu huku wazazi wangu, makaka, madada, wajomba etc.. washachukua chao. Sasa ile natolewa ndani nafika sebleni, nakutana na mwanaume wa roho yangu mwenye sifa nilizozitaka.

"Anaefaa kuishi nami milele na niliye muomba Mungu siyo tu kwa kupiga magoti bali kwa kufunga na ninayeweza kumvumilia! Hapo akiwa ananisubiria.

"Basi nikaulizwa Happy ndo huyu Joseph nikasema Yes!!! Huku akiwa ananiangalia nilivyopendeza mama k wake na kitumbo changu nduuu!!

"Anyways, kama hujakata tamaa na una malengo yako basi usibebe mimba hadi akuoe au hata akutolee mahari na amalize yotee! Tena isichukue miaka utembee na pete ya uchumba hadi ichubue kidole No!

"Siyo mtu hata barua ya posa tu hajaleta kwenu aisee yani huna hata hiyo kumbukumbu halafu baadae uanze kulalamika kwamba ooh tuliishi wote tukazaa mimi ni mkewe oooh shauri yako!! Usifanye mambo kihuni, kuwa na msimamo!

"Ukiamua kuzaa basi uwe umejipanga yani mnunulie mwanao hata kiwanja tu kabisaa. Ndoa hailazimishwi wadogo zangu, wala siyo lazima kama haijatokea! Anaekupenda kweli atakuheshimisha na kukulinda!

"Nipo zangu ofisini naandaa lunch yani full masotojoo!! Ila breakfast ipo tayari RESTAURANT YA KISHUA " ameandika Happy.

Happy ambaye aliolewa na Sugu baada ya kuachana na Faiza ambaye ni hasimu wake mkubwa, haikuchukua muda Faiza amejibu kwa kuandika yafuatayo;

"Dini inasema mumeo akiwa anak*k*la (***) we sio mke tena unaruhuhisiwa kuondoka bila talaka"

"Happy akajibu yafuatayo "sijamaliza kusoma gazeti lako mwanzo tu nimekuona kilaza na hater sasa kwani si nimesema ndoa sio lazima ujipange? Embu njoo huku nikufundishe kupika mchuzi wa nazi."

Aidha, Faiza amesema kuwa Happy huwa anaumia sana Sugu kumlipia ada mtoto aliyezaa nae

Chanzo: www.tanzaniaweb.live