Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamonize amemdunda vibaya Kajala-H Baba

Harmonize, KAJALA NA HBABA Hamonize amemdunda vibaya Kajala-H Baba

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba Harmonize na Kajala wameachana, msanii ambaye aliwahi kuwa chawa wao, H Baba ameibuka na kudai kuwa, jamaa alimdunda mrembo huyo.

H Baba amesema, yeye anafahamu tukio hilo limetokea muda mrefu tu na ndilo lilosababisha wawili hao waachane japo ishu hiyo imekuja kusanuka mapema wiki hii.

"Kitambo tu mbona, Harmonize alimdunda vibaya sana Kajala sasa bibie akaona isiwe tabu kupigwa tena? Jamaa anaendekeza mademu wasio na kichwa wala miguu sasa yule demu wa kwenye video ya ameloa na Kajala nani zaidi?" alihoji H Baba akidai kuwa ugomvi ulianzia baada ya Kajala kugundua mwamba anaruka na mrembo huyo aliyekuwa video queen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live