Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hamisa, Zari kuchuana katika tuzo mhamasishaji bora wa kampuni

Hamisa Pic Data.png Hamisa, Zari kuchuana katika tuzo mhamasishaji bora wa kampuni

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamitindo kutoka nchini Tanzania, Hamisa Mobetto na mjasiriamali Zarina Hassan’Zari’ wanatarajiwa kuchuana katika tuzo za Africa Choice Awards katika kipengele cha mhamasishaji bora wa kampuni.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Oktoba mwaka huu nchini Nigeria ikiwa ni mara yake ya  21 tangu kuanza kutolewa kwake ambapo jumla ya vipengele 32 vitawaniwa.

Tanzania tayari wasanii kumi wametajwa kuwania vipengele mbalimbali, huku Hamisa akiwania kipengele kimoja na Zari.

Wawili hao ni wazazi wenza wa staa wa bongo fleva Diamond Platnumz na kutokana na maisha yao wamejikuta wakizalisha ushindani wa wafuasi katika mitandaoni ambayo imekuwa ikiwasapoti katika mambo mbalimbali, jambo litalosababisha kuwepo kwa mchuano mkali katika upigaji kura.

Ukiachilia Zari na Hamisa, kwenye tuzo hizo pia yupo mrembo Wema Sepetu ambaye naye kwa nyakati tofauti alishawahi kuwa katika mahusiano na Diamond Platnumz na mpaka sasa yeye na Zari haziivi na wamekuwa wakirushiana vijembe mara kwa mara.

Wema yeye anawania kipengele cha mwigizaji bora wa kike akichuana na waigizaji wengine na nchi wanazotoka kwenye mabano akiwemo Zynnellzuh (Ghana), Pearlthusi (South Africa), Lindaosifo (Nigeria), Hlubimboya1 (South Africa),Nomzamom (South Africa) na Lillyafe (Nigeria).

Wengine waliotajwa katika tuzo hizo kutoka Tanzania na vipengele wanavyowania kwenye mabano ni   Idris Sultan mchekeshaji bora, Irene Uwoya na mwanamitindo wa kike, Ben Breaker Chaguo la watazamaji, Diamond Platnumz Msanii wa mwaka ,Millard Ayo mtu mwenye mvuto , Gabo Zigamba mwigizaji wa kiume wa mwaka na muuzaji wa bidhaa za nywele Luluz Hair.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz