Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa: Rick Ross ananipa makopakopa

Mobeto Na Rick ,,,,.jpeg Hamisa na Rick Ross

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisa Mobeto; ni msanii wa Bongo Fleva, muigizaji na mwanamitindo wa nchini Tanzania ambaye anafunguka kuhusu uhusiano wake na rapa wa Marekani, Rick Ross.

Hamisa anasema kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rick Ross au Madevu lakini ni marafiki wakubwa.

“Hakujawahi kuwa na mahusiano. Huwa ananipa makopakopa kwa sababu nafanya naye kazi. Hakuna chochote. Pindi kikitokea kama kuna kitu mtafahamu," anasema Hamisa ambaye ameachia EP yake ya Yours Truly.

Hamisa anasema Rick Ross amekuwa nguzo muhimu katika usanii wake kwa kuwa amekuwa akimsaidia kwa ushauri kwani anavutiwa sana na muziki wake.

“Yeye ni mtu ambaye ananisapoti. Ana moyo wa kusaidia,” anasema Hamisa ambaye pia ni baby mama na ex wa Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live