Menu ›
Burudani
Fri, 10 Apr 2020
Chanzo: mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Amerudi tena. Ndivyo ninavyoweza kusema baada ya msanii Ali Kiba kutoa wimbo uitwao Dodo katika mtandao wa Youtube leo asubuhi Jumatano Aprili 8, 2020.
Hamisa Mobetto ndio aliyepamba video hiyo jambo lililoanza kuibua mjadala mtandaoni kutokana na kuwa mwanamitindo huo ni mzazi mwenzake msanii Diamond Platnumz ambaye ni mpinzani wa Ali Kiba katika tasnia ya muziki nchini Tanzania.
Katika video ya wimbo huo, Kiba anaonekana amevaa kama mfalme na Mobetto amevaa kama malkia na maeneo mengine kama bibi harusi.
Pia Soma
- Alichokisema Sallam kuhusu Diamond
- Ndani ya Boksi: Darassa mpaka ale unga ili tumuelewe?
- DJ SinyorRita ajivunia kuwa na fani ya kipekee
- Mchumba wa Davido akutwa na maambukizi ya corona
Wimbo huo tangu uachiwe ndani ya saa saba ulikuwa umetizamwa na watu zaidi ya 50,000 katika mtandao wa Youtube, huku watu zaidi ya 10,000 wakitoa maoni yao yanayoonyesha kuikubali kazi hiyo kutoka Kings Music.
Miongoni mwa waliotoa maoni ni david curtis aliyeandika “Dah! Hii nyimbo imetulia sana sana. 1-Beat 100% 2-uandishi 100% 3-wahusika 100 %”.
Ali Kiba mara ya mwisho kutoa wimbo ilikuwa Novemba 8,2019 uitwao ‘Mshumaa’.
Chanzo: mwananchi.co.tz