Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Mobetto, Kajala uso kwa uso msibani Chato

Mobeto Kajala Pic Data Hamisa Mobetto, Kajala uso kwa uso msibani Chato

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wasanii Hamisa Mobetto na Kajala Masanja wamekutana uso kwa uso katika msiba wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Wawili hao wamekutana leo Ijumaa Machi 26, 2021 katika shughuli ya Ibada ya kuaga mwili wa kiongozi huyo inayofanyika kwa mara ya mwisho viwanja vya Magufuli wilaya ya Chato, ambapo baadaye anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao katika makaburi ya familia.

Baadhi ya wasanii wameshiriki katika shughuli hiyo wakiwemo Hamisa na Kajala ambao hivi karibuni waliingia katika mgogoro baada ya kusambaa kwa video mbaya ya Paula ambaye ni mtoto wa Kajala.

Video hiyo iliwekwa kwa mara ya kwanza Februari 14,2021 na msanii Raymond Mwakyusa, maarufu Rayvanny katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, ukiwaonyesha wapo katika mapozi ya mahaba na kuibua gumzo.

Katika tukio hilo ambalo wasanii hawa walifika hatua ya kufikishana Polisi, Kajala alimtuhumu Hamisa kuhusika kwa kile alichoeleza siku hiyo alikwenda kuomba atoke na mtoto wake huyo ambaye ana umri wa miaka 19.

Hata hivyo bado sakata hilo liko mikononi mwa Polisi ambao mara ya mwisho walisema bado upelelezi unaendelea.

Katika msia huo Hamisa na Kajala wameonekana kukaa eneo jirani wakifuatilia kwa karibu Ibada, ambapo picha zao zimeonekana kuwa gumzo pia huko mitandaoni.

Ukiachilia Hamisa na Kajala, wasanii wengine waliohudhuria msiba huo ni Diamond Platnumnz, Ali Kiba, Nandy, Harmonize, Wema Sepetu,Lulu Diva, Jacob Steven’JB’, Jux na wengine wengi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz