Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Mobeto atoa ushauri kwa mastaa wa kike wasiwe watumwa wa mapenzi

73810 Hamisaa+pic

Mon, 2 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamitindo na mwanamuziki wa Tanzania, Hamisa Mobetto amewashauri baadhi ya mastaa wa kike nchini humo wasiwe watumwa wa mapenzi kama alivyokuwa yeye.

Amesema kuwa mtumwa wa mapenzi kunarudisha nyuma maendeleo na sasa amejitambua kwani yalimkuta ndiyo maana anapinga baadhi ya mastaa wenzake wenye tabia hiyo.

"Ninaposema utumwa wa mapenzi ni sababu mimi yalishanikuta, nilikuwa sina cha kufikiria zaidi ya mapenzi kwa mtu niliyekuwa naye.”

“Mbaya zaidi ukute mwanaume unampenda ndio kabisa unakuwa haupo kabisa katika ulimwengu wa maendeleo wewe unachowaza ni mapenzi jinsi yanavyokupelekesha, hii mbaya sana na sitaki kurudi huko tena mimi," alisema Hamisa

Aidha Hamisa amesema alipojitambua na kuachana na masuala ya mapenzi amejiona amechelewa kufanya uamuzi baada ya riziki za mambo ya maendeleo zilipoanza kufunga hasa kupata zabuni za Ubalozi katika kampuni tofauti.

Hamisa ambaye alipiga stori na Mwananchi jijini Dar es Salaam hivi karibuni alisema ameamini kuwa ustaa unaangaliwa vitu vingi na watu wanaokuzunguka hivyo ukiutumia vibaya unaweza kujikuta maskini kila kukicha na kudharaulika.

Pia Soma

Advertisement   ?
Hamisa amedai pia mzazi mwenzake wa msanii wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz hakuwa aina ya wanaume ambaye alikuwa ana mwitaji.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz