Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Mobeto aibukia kwa King Kiba

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii Ali Kiba amerusha video ya Hamisa Mobeto akiwa anaimba wimbo wa Masozy.

Hamisa ambaye pia anaimba bongo fleva kwa sasa, ameonekana akiimba wimbo huo akiwa ndani ya gari, huku akicheza kwa mapozi ikiwemo kuzungusha macho yake kushoto na kulia.

Gumzo la video hiyo inachangiwa na Hamisa ambaye ni mzazi mwenzake na msanii Diamond kuipenda nyimbo hiyo huku ikijulikana wazi kuwa Ali Kiba ni mshindani wa Diamond kwenye muziki.

Baadhi ya watu walioiona video hiyo akiwemo How7958, amesema ‘lazima tufukie mashimo.’

Wakati Kinondy9514, amesema ‘Hiki kitu si mchezo mji wa pili wataimba japo kimyakimya’

Wimbo huo wa Masozy ulioimbwa na wasanii wa Kings Music kwa kushirikiana na Ali Kiba, uliachiwa rasmi Desemba 13, 2018.

Kuanzia hapo umekuwa gumzo na utakuwa ni wimbo wa tatu kuachiwa tangu kutambulishwa rasmi kwa kundi hilo Oktoba mwaka 2018.

Kundi hilo linaundwa na wasanii wanne akiwemo Cheed, Killy na K-2GA na mdogo wa Ali Kiba anayeitwa Abdu Kiba.

Nyimbo nyingine walizoachia mbali na Masozy, ni pamoja na ‘Mwambie Sina’ na ‘Toto’.



Chanzo: mwananchi.co.tz