Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Mobeto, Tanasha kuchuana kwenye tuzo Afrika Kusini

70006 Pic+mabeto

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamitindo marufu nchini Tanzania, Hamisa Mobeto na msanii wa Kenya, Tanasha Donna wanatarajiwa kuwania tuzo za starqtawards zitakazofanyika nchini Afrika Kusini Oktoba 26, 2019.

Mobeto akiwa mzazi mwenzie na msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz huku  Tanasha ni mpenzi wa sasa wa Diamond anayetarajia kupata naye mtoto wa kiume hivi karibuni.

Katika tuzo hizo ambazo hii ni mara yake ya sita kufanyika, Mobeto amependekezwa katika kipengele cha mtu maarufu.

Wakati Tanasha yeye kapendekezwa kwenye kipengele cha burudani kama msanii anayechipukia.

Tayari wawili hao kupitia kurasa zao katika mtandao wa kijamii wa Instagram, wameanza kuwafahamisha mashabiki wao  kuwapigia kura mara tu shughuli itakapoanza  Agosti 14,2019 kupitia www.starqt.com.

 “Ni heshima kubwa sana kufikiriwa mtu bora katikati ya kundi kubwa sana la watu bora wengi sana. Nitajitahidi kufanya kila niwezalo kuwa Hamisa bora kwa kadri ya uwezo wangu.”

Pia Soma

“Naomba kura yako kama inavyoonyesha hapo juu, ina maana sana kwangu. Kura zitaanza kupigwa tarehe 14 mwezi wa 8 kupitia tovuti ya www.starqt.com/awards,” amesema Mabeto katika ukurasa wake wa Instagram

Tanasha amewashukuru waandaaji kwa kumpendekeza kuwa mmoja wa washiriki kwenye tuzo hizo na kuvipongeza vituo vya televisheni na redio kwa kuendelea kupiga nyimbo zake na kuwaomba watu mbalimbali kumpigia kura kwa wingi.

Tuzo hizo zinalenga kutambua michango ya watu na makundi mbalimbali katika kazi wanazozifanya ikiwemo za kijamii, burudani, biashara na michezo

Chanzo: mwananchi.co.tz