Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Amrejesha Rick Ross Kwenye Himaya Yake

Mobetto Hamisa Amrejesha Rick Ross Kwenye Himaya Yake

Thu, 3 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya ukimya huku akidaiwa kupigwa teke au kibuti na Rapa wa Marekani, Rick Ross, hatimaye mwanamitindo na msanii wa muziki Tanzania, Hamisa Mobeto ametamba kumrejesha jamaa huyo kwenye himaya yake.

Hii ni baada ya Hamisa ambaye ni mama wa watoto wawili kumuandikia Rick Ross ujumbe mtamu katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa Jumamosi iliyopita.

Kwa mujibu wa ujumbe wa Hamisa, mrembo huyo alikuwa akimtakia Rick Ross kila la heri kwenye kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, lakini timu ya mrembo huyo ikaenda mbali zaidi kwa kuonesha furaha kufuatia Hamisa kuweza kumrejesha mwamba huyo kwenye himaya yake.

Wengi wa timu Hamisa, sasa wanaamini ni kweli kwamba Hamisa na Rick Ross ni wapenzi, lakini wapo wanaoonesha shaka kwamba huwenda ni urafiki wa kawaida tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live