Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Kopwe arejea baada ya Miss World

Rdrdr Halima Kopwe arejea baada ya Miss World

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshiriki wa Miss World 2024 kutoka Tanzania Halima Kopwe, ambaye ni Miss Tanzania 2022 amerejea nchini hii leo akitokea nchini India katika mashindano ya 71 ya Miss World.

Halima amefika na kupokelewa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na alipofika amefunguka kujivunia kuiwakilisha Tanzania kwenye hatua mbali mbali.

Halima alikuwa miongoni mwa washiriki 112 na alifika hadi hatua ya 40 Bora kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Machi 9,2024, Mumbai, India.

Taji la Miss World mwaka huu 2024, limeenda kwa mlimbwende Krystyna Pyszková wa Czech Republic.

Leo Machi 11 pia usisahau, ni siku ambayo mlimbwende Halima Kopwe anasherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa na kuongeza mwaka mwingine.

Una chochote cha kumwambia?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live