Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya Mwana FA baada ya kuchukuliwa vipimo vya Corona

99619 FA+PIC Hali ya Mwana FA baada ya kuchukuliwa vipimo vya Corona

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam Sharaf kujitokeza na kueleza kuwa ameambukizwa corona mwanamuziki Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ naye ameeleza kuwa amekutwa na virusi vya corona lakini yuko vizuri kiafya. Kupitia video aliyorekodi Mwana FA ameeleza kuwa siku chache zilizopita alikwenda nchini Afrika Kusini na wakati anarudi alianza kujihisi kuwa na homa kali. Hali hiyo ilifanya kwenda hospitali na kutaka apimwe kubaini kama ana corona na majibu yametoka leo yakionyesha kuwa ana ugonjwa huo. “Nilijitenga kuhakikisha siathiri watu wengine nimefanya vipimo na nimekutwa positive. Niwaambie kuwa ugonjwa huu upo na unaweza kumpata mtu yeyote, tujihadhari,” amesema FA. Aliwaasa wananchi kuwa hata ikitokea wameupata usishtuke wala sio kitu cha kutisha maana ukipata huduma virusi wake wanakwisha baada ya siku saba hadi 10.

Chanzo: mwananchi.co.tz