Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna uzito wa mashairi kama yangu uliotokea katika taifa hili – Afande Sele

1486 20838605 284243888649901 8530835141927370752 N E1516259241159 TZW

Thu, 18 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii Mkongwe wa Bongo Flava, Afande amefunguka sababu ya kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma mpya.

Mkali huyo wa rhymes ameiambia Planet Bongo ya EA Radio yupo mbioni kutoa ngoma mpya kwani watu wake wanamuulizia sana kutokana na uzito wa mashairi yake.

“Mimi nina nyimbo nyingi zilizo bora isipokuwa nawaomba wanipe muda nafaikiri kabla ya Pasaka nitatoa wimbo mpya kwa ajili yao kwa sababu maombi yamekuwa mengi na nidhani wamekosa mawazo yangu na hakuna uzito wa mashairi kama yangu uliotokea katika taifa hili,” amesema Afande Sele.

Ameongeza kuwa muziki umekosa mtu wa aina yake na kilichomkimbiza katika game ni kushauriwa kufanya muziki wenye swag ambao yeye hauwezi.

Ngoma ya mwisho Afande Sele kutoa na kufanya vizuri inakwenda kwa jina Dini Tumeletewa ambayo alimshirikisha Belle 9.

Chanzo: bongo5.com