Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Haji Manara amvalisha pete ya uchumba Zaylissa

Manara Na Zay Haji Manara amchumbia Zaylissa.

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara amvisha pete ya uchumba mpenzi wake Zaylissa siku ya jana Januari 18, 2024

Sherehe hiyo ya kuvishana pete ilienda sambamba na kusherehekea kumbukizi ya siku ya  kuzaliwa Haji, ambapo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Aunty Ezekiel, Arene Uwoya, Diamond, Lamata, Nandy na  Ommy Dimpoz.

Katika sherehe hiyo Haji ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa anaomba sana dua za mashabiki wake  kwani anatamani ndoa anayotarajia kufunga na Zay iwe ya mwisho kwake.

Zay na Haji walianza kuhusishwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mapema Novemba mwaka jana, ingawa mwanzo waligoma na kudai kuwa wapo kwenye urafiki wa kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live