Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara ajiweka kwa Kajala

Manara Ersss Haji Manara ajiweka kwa Kajala

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ndoa zake zote mbili za mwisho kupasuka ndani ya muda mfupi, Haji Manara aanza kujikomba kwa Kajala kisha kuwatungua kinadada wengine.

"Achana na kila kitu kuhusu Kajala, ila kwenye hili nakupenda bure my sister, upo very serious na mazoezi, unajijali mno afya yako, nimelipia wanawake wengi gym lakini wengi kama siyo wote wameishia njiani, wanaenda kujisnap siku mbili tatu, kisha wanayeya," ameandika Manara anayesifika kwa uongeaji.

"My sister unautengeneza mwili na afya yako kwa maumivu ya kutosha na hautanii love, una rika sahihi na jinsi ulivyo hauna kisu hata kimoja cha kutengeneza hipsi wala kota.

"Imagine hawa mpata mpatae wa mjini wakifika umri wako watakuwa nyang'anyang'a, hawapumnziki hawafanyi training, hawali vizuri zaidi ya michips kuku na mitomato pori, kutwa wanashinda Mbwikidi kupiga ndui za pombe" amesisitiza Manara

"Ahhh ngoja nikutafute tuyajenge dada yangu kipenzi, najua mimi na wewe tunashabikiana kinoma," amemalizia Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live