Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara ajitosa kwenye uigizaji

68404 Pic+manara

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msemaji wa klabu ya Simba nchini Tanzania, Haji Manara amejitosa kwenye tasnia ya filamu huku akieleza mkataba wake Simba haumfungi kufanya hivyo.

Manara ameonekana wiki hii akiwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Movie visiwani Zanzibar jambo lililoisukuma Mwananchi kutaka kujua sababu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Julai 26,2019, Manara ambaye amekuwa msemaji wa Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania 2018/19 kwa miaka zaidi ya minne sasa, amesema yupo  visiwani  huko wakipika filamu.

“Niliombwa na mtandao wa Swahiliflix ambao utaanza kusambaza kazi za filamu za bongo hivi karibuni kutengeneza maudhui kwa kuniona nafaa, ndio maana mmeniona niko huku Zanzibar tukilikamilisha hilo,” amesema

Alipoulizwa kama mkataba wake Simba haumnyimi kufanya hayo, anesema kufanya kwake kazi Simba hakumzuii kufanya mambo mengine.

 

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz