Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ameamua kusherehekea kwa pamoja na wake zake wawili hotelini na kusema kuwa ni siku kubwa sana kula chakula na wake zake kwa upendo na furaha.
Hatua hii imekuja ikiwa ni siku chake tangu amefunga ndoa na aliyemtambulisha kuwa ni msaidizi wake Bungeni jijini Dodoma.
Hivi karibuni kuiibuka maneno ya chini chini kuhusiana na wake wa Haji Manara kutokuelewana, msemaji huyo jana akaamua kuvunja ukimya na kuadhihirishia umma kuwa kwasasa wake zake wote wawili wamepatana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Haji alipost picha akiwa na wake zake picha hizo zikiambatanishwa na ujumbe ukiwa unaeleza kuwa;
“Siku kubwa sana kwangu na kwa Wake Zangu Wapendwa, Baada ya Kula Chakula Cha Pamoja Usiku huu Hyatt Kenpinsk, Was Superb Dinner na Sasa Tunakwenda kujenga familia” ameandika Manara
Hii inamaana kuwa msemaji huyo amemaliza tofauti zake na wake zake, haya mwanangu sana dondosha komenti yako hapo chini na utujuze, je wewe unamalizaga vipi tofauti na wake zako?
"Siku kubwa sana kwangu na kwa Wake Zangu Wapendwa, Baada ya Kula Chakula Cha Pamoja Usiku huu Hyatt Kempinsk. Was Superb Dinner na Sasa Tunakwenda kujenga familia. Mipicha Picha na Video nyingine kesho Insha'Allah" ameandika Manara mtandaoni.