Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara afunga ndoa tena

Hajismanara 16500090113920 Haji Manara afunga ndoa

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa klabu ya #YangaSC, Haji Sunday Manara amefunga ndoa na mwanadada anayefahamika kwa jina la Rubynah Salum mara baada futari ya jana Alhamisi, Aprili 14 2022.

Ndoa imehudhuriwa na aliowaalika tu ambapo miongoni mwa walioalikwa ni, Hamisa Mobetto, Esha Buheti na mtangazaji Zamaradi Mketema. Wengine walioalikwa katika shughuli ya ndoa hiyo viongozi kadhaa wa klabu ya Yanga na marafiki zake wachache.

Katika ndoa hiyo iliyofungwa na mwanamke ambaye kwa taarifa za awali inaelezea kuwa ni aliyekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda sasa.

Ikumbukwe kuwa usiku wa Desemba 10, 2020 Manara alifunga ndoa na Naheeda Abdallah baada ya kuachana na mkewe wa kwanza, lakini miaka michache baadaye ndoa ya Manara na Naheed ikadaiwa kuvunjika kutokana na migogoro ya kifamilia lakini taarifa hizo hazijawahi kuthibitishwa na wawili hao ama wanafamilia.

Hivyo mpaka sasa haijafahamika iwapo bado anaishi na Naheed ambaye ndoa yao ilivunja rekodi ya mauzo na hakimiliki za maonyesho kununuliwa na Azam TV, ama wameachana na huyu aliyemuona jana ni mke wa pili au lah!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live