Siku ya tarehe 8 itakuwa siku ya kumuombea dua aliyekuwa msanii wa Bongo fleva Marehemu haithamkim na pia kusheherekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao mpendwa Anaiyah.
Kupitia ukurasa wa instagram wa haithamkim ambaye kwa sasa ni marehemu, umepostiwa ujumbe unao someka hivi.
"Tunapenda kuwakaribisha kwenye tukio muhimu siku ya tarehe 8. Tutaungana pamoja kufanya dua kwa ajili ya marehemu mke wangu mpendwa, na pia kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wetu mpendwa Anaiyah Ni wakati wa kutoa heshima, kukumbuka na kusherehekea maisha ya mke wangu Haitham Kim ambaye ametuacha.
"Tunakualika kuungana nasi katika dua hii maalum ili kumuombea amani na utulivu wa milele. Pia, tutasherehekea siku ya kuzaliwa ya Anaiyah kwa furaha na upendo, tukiadhimisha maisha yake na kumtakia heri tele katika safari yake ya maisha.Tafadhali jiunge nasi tarehe 8 kwenye tukio hili maalum. Tunathamini sana uwepo wako na msaada wako wakati huu wa kipekee.
"Tukio hili litafanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu mke wangu Kiwalani. Asanteni"
Haitham alifariki mwezi uliopita kutokana na kusumbuliwa na tatizo la upumuaji. Pumzika kwa amani Haithamkim.