Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H Baba ataja sababu kwa nini haziivi na Kajala

H BABA NA KAJALA H Baba ataja sababu kwa nini haziivi na Kajala

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisi Ramadhan Baba ‘H Baba’ ameweka wazi kuwa hana tatizo lolote na muigizaji Kajala Masanja lakini hawezi kuwa karibu naye maana yupo kwenye mahusiano na mtu ambaye alitaka kumfelisha maishani.

H Baba amefunguka hayo alipokuwa akijibu maswali aliyoulizwa na mtangazaji wa Wasafi FM, Diva The Boss aliyekuwa anataka kujua uhusiano wake na muigizaji huyo.

“Sina tatizo lolote na Kajala. Hatuongei kwa sababu, yupo kwenye mahusiano na mtu ambaye alitaka kubadilisha maisha yangu kuwa mabovu ili afurahie,” alisema H Baba.

Licha ya kutomtaja jina mwanamume wa Kajala anafahamika kuwa ni staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na inakumbukwa msanii huyo aliwahi kumchukua H Baba na kuwa karibu naye kikazi lakini hata hivyo baadaye wakatofautiana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live