Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H Baba asimulia mkewe Flora Mvungi alivyochepuka na kuzaa nje ya ndoa

H Baba Na Mkewe H Baba asimulia mkewe Flora Mvungi alivyochepuka na kuzaa nje ya ndoa

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisi Ramadhan Baba ‘H Baba’ amesimulia jinsi mkewe Flora Mvungi alivyomsaliti wakiwa angali kwenye ndoa.

H Baba amesimulia hayo usiku wa Agosti 17, 2022 alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi FM ambapo alieleza suala hilo lilitokea miaka kadhaa iliyopita wakati yeye akiwa jijini Mwanza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

“Mimi nilikuwa nimekwenda Mwanza kujenga nyumba na nilipokuwa narudi Dar, nikapata taarifa kwamba mke wangu ana mwanaume mwingine. Nikamtumia meseji, kwamba naondoka lakini ahakikishe tu wanangu hawasumbuliwi na huyo mwanaume wake,” anasema H Baba.

Mkali huyo wa Bongo Fleva anasema tangu hapo, aliamua kukaa pembeni na wakawa wanawasiliana tu kwa ajili ya matumizi ya watoto.

“Siku moja nikiwa na mama Mwanza, nikampigia video call na hapohapo mama alipomuona akaniambia kwamba mke wangu ana mimba na ukizingatia sikuwa naye hivyo ilikuwa ni ya mwanaume mwingine,” anasema H Baba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live