Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H.Baba amjibu mkewe ishu ya kutohudumia watoto

Flora Mvungi We H.Baba na Flora

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, H.Baba amefunguka namna alivyochukizwa na kitendo cha aliyekuwa mkewe Flora Mvungi kuandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram siku wiki kadhaa zilizopita akidai msanii huyo hawahudumii watoto wake.

Flora aliandika: "Unajiita baba halafu wanao wanalelewa ukweni. Pambana wewe! Baba sio jina la ubatizo mfyuuu".... ilisomeka sehemu ya ujumbe huo mrefu wa Flora kupitia ukurasa wake ambao ni wazi kuwa ulienda kwa mzazi mwenzie H.Baba waliyepata nae watoto wawili.

H.Baba amekiita kitendo hicho ni ukosefu wa heshima na nia ya Flora ni kutaka kumkomoa. H.Baba pia amebainisha kuwa hajawai kumpa talaka Flora Mvungi, licha ya sasa kuwa ni walezi tu kwa watoto wao.

Mbali na hilo, H.Baba amewachana baadhi ya wasanii wakike Bongo wenye tabia za kuharibu ndoa/mahusiano ya watu ambao ndio walioharibu mahusiano yake na Flora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live