Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H.Baba: Nimechoka kudanganya, nimefirishika

H Babababa H.Baba.

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Hamisi Ramadhan Baba 'H Baba' amesema kuwa amechoka kudanganya watu kuwa ana mali, kwani ukweli ni kwamba amefirisika na hana pesa kabisa.

Akizungumzia hilo, H.Baba ambaye ni chawa wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema;

"Nilikuwa nadanganya sina mali zozote nimefilisika, muziki umenifilisi nimeuza mali zangu zote, nilikuwa na mpango wa kutoa wimbo na Diamond Platnumz pamoja na Alikiba lakini nimeshindwa kwasababu sina pesa.

"Nimekuwa nikiwekeza pesa nyingi kwenye muziki lakini pesa hairudi, nimechoka kuwadanganya sina mali yoyote nimeisha," amesema H.Baba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live