Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H Baba: Ndoa yangu na Florah Mvungi bado ipo

46563 Pic+h+baba H Baba: Ndoa yangu na Florah Mvungi bado ipo

Wed, 13 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nani anasema ukweli? Ndilo swali wanalojiuliza sasa mashabiki wa wanandoa H Baba na Florah Mvungi mmoja akisema wameachana na mwingine anadai hakuna kitu kama hicho.

Florah ambaye ni mwigizaji wa filamu aliyejizolea umaarufu kupitia mchezo wa Bongo Dar es Salaam, aliimbia Mwananchi jana Machi 12, kuwa aliachana na mumewe H Baba miaka mitatu iliyopita lakini hawakutaka kuliweka hilo wazi kwa sababu ambazo alidai ni siri yao.

Mwananchi imezungumza  H Baba ambaye kwa sasa makazi yake yapo mkoani Mwanza na amesema anamtambua Florah kuwa mke wake halali tangu walipofunga ndoa mwaka 2013.

Akizungumza leo Machi 13, 2019, H Baba aliyewahi kutamba na muziki wa aina ya Bongo Bolingo, amesema hawezi kuachana na mkewe kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram au vyombo vya habari kwani ndoa yao walifunga kwa kufuata taratibu zote za dini na kifamilia.

“Siwezi kuachana na mke wangu Instagram, kama nilivyofuata taratibu wakati namuoa ndivyo nitakavyofanya ukifika wakati wa kuachana naye lakini mtambue kwamba Florah bado ni mke wangu na ninampenda sana.

 “Hayo mambo yao ya Bongo Dar es Salaam ya kuzungumzia mpaka masuala ya familia kwenye mitandao huwa siyapendelei na sijalelewa hivyo muulizeni vizuri awaonyeshe talaka,” amesema H Baba aliyewahi kutamba na nyimbo Mpenzi Bubu na Poteza.

Soma zaidi: Florah Mvungi: Ndoa yangu na H Baba ilivunjika miaka mitatu iliyopita



Chanzo: mwananchi.co.tz