Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

H.Baba: Mtoto wangu anafanana na Uwoya

Hbabs 615235 H.Baba: Mtoto wangu anafanana na Uwoya

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

H.Baba anadai Mtoto wake wa kike aitwaye Tanzanite aliyemzaa na Mwigizaji wa filamu Florah Mvungi anafanana na Irene Uwoya ambaye ni Mpenzi wake wa zamani.

"Maswali yenu ya DM kunifatafata nimemuuliza na mimi huyu mtoto kwanini anafanana sana na Uwoya kila anavyokuwa ananishangaza. ntamuuliza mshikaji wangu Uwoya na kwanini Krish na Tanzanite wanataka kufanana

hivi kuna nini hapa au duniani wawili wawili Asante UWOYA asante FLORAH huyu TANZANITE sijui au mimi nilibaki na chembe chembe za UWOYA kwanini hivi? Asante Mungu Nina mbegu kali za watoto wazuri sigawi mbegu hovyo tafadhali nimemzaa Uwoya uku tuongee ukweli huyu mtoto ni TANZANITE kweliii.

"Mwanangu umefanana sana na Uwoya au mimi naona vibaya mtanisamehe sana huyu(Tanzanite) ndie mtoto pekee alizaliwa na nyota yake ya kupendwa sio yakulazimisha.

"Asante FLORAH huyu mtoto kanifundisha kitu inabidi nichunge sana mbegu zangu zina afya bora nakutengeneza watoto wazuri warefu.

"Kuna mtu kanuna kusikia hivyo atatukana ndio hivyo sijui nifanye biashara yakupandikiza mbegu kama unataka mtoto kama huyo unanilipa nakupa mbegu unapeleka uko naona kama bora nifanye hivyo au mnasemaje walimwengu?" amesema H.Baba.

Ikumbukwe kwamba kipindi H.Baba anafanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Flava aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Irene Uwoya mara baada tu ya kumaliza kushiriki Miss Tanzania lakini baadaye wakaachana.

Baadaye H.Baba akafunga ndoa na Florah Mvungi aliyewahi pia kuwa Miss Pwani na kushiriki Miss Tanzania, walipata watoto wawili akiwemo Tanzanite huyu anayedaiwa kufanana na Uwoya lakini ndoa yao ilivunjika.

Hii si mara ya kwanza kwa H.Baba kuzungumzia Irene Uwoya kwenye mitandao ya kijamii na amekuwa akifanya hivyo mara nyingi lakini Uwoya hajawahi kuzungumzia wala kujibu chochote kile kuhusu H.Baba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live