Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gumzo ukimya wa Bifu la Drake, Kendrick Lamar

Drake X Kendrick Gumzo ukimya wa Bifu la Drake, Kendrick Lamar

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zimepita wiki mbili sasa tangu kuwe na ukimya wa muendelezo wa bifu kati ya Rapa Drake na kendrick lamar na wafuasi wa vita hiyo kuamini huenda bifu hiyo imeisha rasmi.

Huenda bifu hiyo ikaibuka tena mara baada ya Rapa Drake kumchana kwa maneno makali mtayarishaji wa muziki “Metro Boomin” kwenye wimbo unafahamika kwa jina la “U My Everything” aliyoshirikishwa na bi dada Sexyy Red, Drake ametumia maneno makali ya kumdhihaki ki mwili mtayarishaji metro boomin

Wakati bifu ya Drake na kendrick ilipokuwa inaendelea Mtayarishaji Metro aliachia mdundo mitandaoni alioupa jina la “BBL Drizz” na kuruhusu wachanaji wautumie ikiwa kama “Diss beat” kwenda kwa drake na sasa Drake amejibu mapigo.

Nikukumbushe kuwa bifu ya Drake na kendrick ilianzia kupitia wimbo wa Metro na Future walimshirikisha kendrick unajulikana kama “Like That” ambapo Kendrick alitumia Vesi yake kuwachana Drake na J cole

Chanzo: www.tanzaniaweb.live