Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Guchi afanya balaa, aachia mikwaju miwili kwa mpigo

Guchi Guchi afanya balaa, aachia mikwaju miwili kwa mpigo

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki kutoka Nigeria anayesumbua vichwa vya wasanii wengi kwa kizazi kipya kwenye Afrobeat, Guchi ameachia vyuma vizito viwili ambavyo ni ALL OVER YOU na MON BEBE, ambapo ALL OVER YOU imetengenezwa na Shugavybz huku MON BEBE ikiwa imetengenezwa na Kaelbeatz.

Ngoma hizi ambazo zinazungumzia mapenzi zimejawa na story tofauti ambapo kwenye ngoma ya ALL OVER YOU anazungumzia mahusiano yalivyo mlewesha na yupo tayari kupambana na kushikamana hadi kufa kwenye mahusniano hayo,

Kwa upande wa ngoma ya MON BEBE ambayo imetayarishwa na Kaelbeatz, Guchi ama unaweza muita Purple girl… anaelezea utamu anaoupata kwa mpenzi wake ikiwemo kupata vipele vidogo vya mapenzi kila anapomuona. Kwenye ngoma zote mbili mrembo huyo ni kama anatoa story ya mfululizo ya mapenzi iliyopo juu yake.

Kitendo hiki cha Guchi kuachia kazi zote mbili kumetajwa kuwa ni cha upendo kwani anaweza kufanya kama alivyofanya 2022 kwenye EP yake ya PURPLE DIARY? Au la amewatunuku tu mashabiki zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live