Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grand P ateuliwa kuwa balozi wa Guinea huko Mali

Grand Boyyy Grand P ateuliwa kuwa balozi wa Guinea huko Mali

Sun, 25 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Grand P; ni staa maarufu wa muziki mwenye umbo dogo kutoka nchini Guinea ambaye vyanzo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba, ameteuliwa kuwa balozi wa utamaduni na utalii na Serikali yake.

Grand P kupitia ukurasa wake wa Facebook ametangaza kwamba Kanali Mamadi Doumbuya ambaye anashikilia wadhfa wa Urais wa mpito kufuatia mapinduzi ya Serikali miezi kadhaa iliyopita, amemteua kama balozi wa utamaduni na utalii kwenda kuliwakilisha Taifa hilo kwenye nchi jirani ya Mali.

"Asante kwa Mheshimiwa Rais wa Mpito kwa kuzingatia Mali na Guinea ni mapafu mawili ya mwili mmoja. Heshima zote kwangu kuiwakilisha nchi yangu kama balozi wa utamaduni katika nchi ndugu Mali nikishirikiana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea," amesema Grand P.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Taifa ya Utalii ya Guinea, Kanali Mamadi Doumbuya; Rais wa Mpito ameripotiwa kumpatia Grand P pasipoti ya kidiplomasia kwa ajili ya kazi yake kama balozi wa utamaduni wa Taifa hilo nchini Mali.

Grand Palimshukuru Mkurugenzi Mkuu na kusisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa ajili ya kukuza Utamaduni na Guinea kama kivutio cha watalii.

Jina halisi la Grand P au Big P ni Musa Sandian Kaba na amezaliwa mwaka wa 1990 huko Sanguiana, eneo la Kankan nchini Guinea.

Baadhi ya watu wamekuwa wakimzungumzia maumbile yake yasiyo ya kawaida ambapo anaonekana kama mtoto muda wote na gumzo hilo lilizidishwa hata zaidi baada ya kuweka wazi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo kutoka lvory Coast, Eudoxie Yao ambaye ni mkubwa zaidi kwa muonekano wa mwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live