Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grand P anaswa na kifaa kipya

Grand P.jpeg Grand P

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Grand P; ni staa mwenye mvuto wa kipekee na bilionea nchini Guinea ambaye amenaswa na kifaa kipya anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa.

Hii imeibua minong’ono kwani miezi mitano iliyopita alimvisha pete ya uchumba mwanadada Eudoxie Yao live kwenye runinga hivyo watu wanahisi tayari uchumba wao umesambaratika.

Ikumbukwe, mwaka jana Eudoxie Yao alisema ameamua kuachana na Grand P kwani alimsaliti kwa kuchepuka na mrembo mwingine ambaye siyo huyu wa sasa. Hata hivyo, haukupita muda mrefu picha ya mrembo aliyedaiwa kuchepuka naye ikasambaa.

Baada ya muda, ilielezwa kuwa, Grand P alimuomba msamaha Eudoxie wakarudiana ambapo miezi mitano iliyopita alimchumbia live runingani, lakini kwa sasa habari ya moto ni kwamba jamaa huyo ameonekana kimahaba akiwa na mrembo huyo mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live