Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grand P amvisha pete ya uchumba Eudoxie Yao

Grand P Na Demu Wake 2 Grand P amvisha pete ya uchumba Eudoxie Yao

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Grand P ni staa wa muziki, maigizo na vichekesho ambaye ni maarufu mno mitandaoni (sosholaiti) mwenye utajiri mkubwa kutoka nchini Guinnea.

Amekuwa akizungumzwa zaidi kutokana na maumbile yake kudumaa (dwarf) kisha kujihusisha kimapenzi na wanawake wakubwa na wenye minyamanyama kama yote akiwemo mwanamitindo Eudoxie Yao wa Ivory Coast.

Sasa taarifa ikufikie kwamba, mwamba huyo amepiga goti na kumchumbia Eudoxie; tukio ambalo limerushwa mubashara runingani.

Katika video ya tukio hilo, Grand P anaonekana akimshikilia mkono Eudoxie na kwenda chini kwa goti moja huku akitoa ombi lake la ndoa kwake katika lugha ya Kifaransa.

Eudoxie amefurahia ombi hilo na kuonekana akimuinua, akidokeza kwamba ana kazi ya kuifanya katika kufikia maamuzi ambayo hatayajutia mbeleni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live