Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grand P, Yao ndio basi tena

Grand P Grand P, Yao ndio basi tena

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo mwenye shepu matata kutokea nchini Ivory Coast Eudoxie Yao amemtakia kila la kheri katika maisha aliyekuwa mpenzi wake Grand P, baada ya kumuona kwenye video akijivinjari katika kwenye bwawa la kuogelea na mwanamke mwingine.

Katika video hiyo, mwanamuziki huyo kutoka Guinea mwenye umbile dogo zaidi ameposti video Facebook akiwa amejiachia na mrembo wake mpya.

“Maisha ni kitu cha kuvutia sana, jibambe kadri ya uwezo wako. Mimi najivinjari kivyangu,” aliandika Grand P

Katika comment aliyekuwa mpenzi wak, Eudoxie Yao ameandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri katika Maisha.

Fununu za kuachana kwa wawili hao zilizuka wakati wa mashindano ya AFCON nchini Cameroon mapema mwezi Februari wakati mwanaume huyo mdogo alipoonekana akiwa na wanawake wengi jambo linalotajwa kumkera Yao na kumpelekea kufanya maamuzi ya kumuacha Grand P.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live