Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grand P Anajitakia Mwenyewe

Grand P Grand P na Eudoxie Yao

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

GRAND P ni staa mkubwa wa muziki na mitandao ya kijamii kutoka nchini Guinea ambaye ana tatizo la udumavu wa mwili, lakini anashangaza wengi kwa kupenda kuchukua wanawake wenye miili mikubwa kwa zaidi ya asilimia 100 ukilinganisha mwili wake.

Akiwa kwenye ziara ya kimuziki nchini Cameroon kulikokuwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Grand P aliachia picha akiwa na wanawake wenye mizigo mikubwa na kutangaza kuwa kuanzia sasa ni balozi wao.

Hata hivyo, tukio hilo linajitokeza miezi kadhaa tangu Grand P alipogombana na mpenzi wake Eudoxie Yao akimtuhumu mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia kuwa amemnyang’anya tonge mdomo kabla ya kurudiana.

Tabia yake hiyo ya kupenda wanawake wenye misambwanda inaelezwa kuwa ndiyo humuingiza kwenye matatizo na mpenzi wake hilo, jambo ambalo linasemekana anajitakia mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live