Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Grace Mapunda awapa neno wanawake

GRACE MAPUNDA Grace Mapunda awapa neno wanawake

Thu, 23 Jul 2020 Chanzo: mtanzania.co.tz

Na GLORY MLAY

MWIGIZAJI mkongwe nchini, Grace Mapunda, amewakata wanawake waendelee kufanya kazi kwa bidii na waache kubweteka kwani tabia hiyo ni sawa na kununua umasikini.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, Grace Mapunda anayetamba kwenye tamthilia ya Huba kama Tessa, alisema wanawake wa zamani walikuwa wanategemea zaidi waume zao tofauti na sasa ambapo wanawake wanapaswa kupambana.

“Wanawake wanaokaa bila kujishughulisha na kuukubali umasikini kiukweli wananiumiza sana kichwa, sipendezwi na tabia hiyo, maisha ya sasa yamebadilika hakuna mtu anayependa ategemewe kama zamani, wote inatupasa tuutokomeze umasikini,” alisema Grace.

Chanzo: mtanzania.co.tz