Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gozbert aeleza alichozungumza mara ya mwisho na Magufuli

Gosbet Pic Data Gozbert aeleza alichozungumza mara ya mwisho na Magufuli

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa muziki wa Injili, Goodluck Gozbert ameeleza kauli ya mwisho aliyozungumza na aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

 Akizungumza na MwanaSpoti, Gozbert amesema anakumbuka ilikuwa Aprili mwaka 2018 alipomualika katika uzinduzi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete kutumbuiza, Ikulu Dar es Salaam.

Baada ya hafla hiyo alisema alipata wasaa wa kuzungumza na kiongozi huyo na kati ya mambo aliyemuambia ni kumpongeza na kumwambia aongeze bidii zaidi.

“Maneno ambayo Rais aliniambia kiukweli yamekuwa yakijirudia mara kwa mara masikioni mwangu na hata sasa baada ya msiba kila ninapokumbuka tukio lile,”amesema Gozbert.

Hata hivyo msanii huyo amesema anashukuru baada ya mualiko ule alijikuta akipata heshima kubwa ambayo hata sasa inaishi katika maisha yake na imebaki kuwa kumbukumbu kwake hata sasa,”alisema.

Pia haukuishia hapao kwani siku mbili baada ya ule mualiko, kiongozi huyo alimpigia simu na kumpongeza kwa album aliyompatia kama zawadi na kufurahi kwa kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kiongozi mkubwa wa nchi kama yeye angeweza kuwa shabiki wa muziki wake.

Related



VIDEO: Diamond aeleza alivyoulizwa na Magufuli kuhusu siri ya baba yake mzaziMambo ambayo kwake yameacha alama kubwa katika muziki wake,” alisema

“Nilimpenda sana baba yangu huyu kifo chake kiukweli kimeniumiza sana kwani nimepoteza rafiki, kiongozi ambaye ameacha alama kwenye maisha na muziki wangu ,” ameongeza Gozbert.

Kufutia kifo chake hicho, amesema aaendelea kuomba Kwa ajili ya familia yake, ili Mwenyezi Mungu awape faraja katika nyakati hizi ngumu.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz