Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Good News! Kylie Jenner abahatika kujifungua mtoto wa kike

2610 Screen Shot 2018 02 05 At 8.12.12 AM 598x400.png

Mon, 5 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Story inayochukua headlines nchini Marekani ni kuhusu Kylie Jenner ambao wengi wamemfahamu kupitia umaarufu alionao dada yake Kim Kardashian na familia nzima ya Kardashians.



Ni miezi kadhaa imepita toka tetesi za Kylie Jenner kusambaa kuwa ni mjamzito katika mitandao ya kijamii ingawa yeye mwenyewe hakuwahi kulithibitisha  hilo mahali popote.



 

Kupitia instagram account ya Kylie Jenner ametangaza furaha aliyonayo baada ya kujifungua salama mtoto wa kike siku ya February 1,2018 ikiwa baba wa mtoto huyo ni rappa wa Marekani Travis Scott.

“Samahani kwa kuwaweka kwenye giza na kupata mitazamo mbalimbali, nilitambua kuwa nilihitaji maisha chanya kwaajili ya mtoto wangu, sikutaka apate stress ndio maana nikafanya hivyo.

“Nawashukuru marafiki na familia yangu kwa kuficha hii siri, mtoto wangu mzuri na mwenye afya amezaliwa February 1,2018 sikuweza kusubiri kuwatangazia baraka hizi, Asanteni kwa kunielewa”





Tunda “Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari ili niongee naye nini?”

Chanzo: millardayo.com