Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Godliver ajivunia tuzo ya Msanii Bora wa Kike

Msanii Godliver Godliver ajivunia tuzo ya Msanii Bora wa Kike

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa sinema za Kibongo, Godliver Gordian amesema anajivunia kushinda tuzo ya msanii bora wa kike 2021.

Akizungumza na Wasafi TV, Godliver amesema tuzo hizo za Filamu Tanzania zilioandaliwa na Serikali zilikuwa ni za kwanza hivyo imetoa chachu kubwa kwa wasanii.

“Sasa hivi sit u kwamba natambulika kama msanii bali natambulika kama msanii niliyeshinda tuzo. Imeongeza kitu kwenye kazi yangu, watu pia wanapenda kufanya kazi na mtu mwenye taito,” alisema Godliver.

Alipoulizwa kuhusu changamoto za tuzo hizo na nini anashauri kwa waandaji, Godliver alisema anaamini waandaji wanafahamu wapi kulikuwa na changamoto na wataboresha kwa mwaka huu.

“Tunajua kwamba kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza, waandaaji watakuwa wame-note down changamoto na watazifanyia kazi mwaka huu,” alisema Godliver.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live