Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gnako asema EP yake ni moto

E6c84a5c0b29db3e82f50d89be605851.jpeg Gnako asema EP yake ni moto

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BAADA ya kusikia EP za wasanii mbalimbali staa wa muziki wa Bongo flava, wa kundi la Weusi, George Mdeme ‘Gnako Wara Wara’ , amesema wasubiri kuna kazi nzuri anatarajia kuachia ambayo itasimamisha nchi.

Alisema EP bado hajaipa jina lakini inatarajiwa kuwa na nyimbo tano ambazo anaamini zitakuwa bora na zitakata kiu ya mashabiki wake ambao wana hamu na kazi mpya kutoka kwake.

Akizungumza na gazeti hili Gnako, alisema wasanii wengi wa Bongo flava, wameachia nyimbo nyingi nzuri siku za karibuni na kuongeza ushindani mkali katika kiwanda cha muziki lakini yeye amekuja kuleta kitu tofauti ambacho kitakuwa gumzo.

“Sio kwamba nawatisha lakini nataka niwaambie kuwa kama kuna mtu alikuwa ana mpango wa kuachia nyimbo ni bora aitangulize ngoma yake mapema sipendi lawama.

“Nilikuwa kimya kwa muda mrefu nikiandaa kazi hii ambayo sasa iko mbioni kukamilika nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula muziki mzuri unakuja muda si mrefu,” alisema Gnako.

Chanzo: www.habarileo.co.tz