Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gigy asimulia chanzo ugomvi wake na Diva

Gigy Na Diva Gigy asimulia chanzo ugomvi wake na Diva

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameanika chanzo cha ugomvi wake na mtangazaji Loveness Malinzi ‘Diva’ ni chuki binafsi ambazo ziliibuka ghafla bila kuelewa chanzo chake ni nini.

Gigy amesimulia inshu hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV ambapo alianza kwa kusimulia jinsi walivyokutana hadi walipofikia hatua ya kuzinguana.

“Nilikutana naye mtandaoni. Alinichek you are so real. Nikaomba kuonana naye mimi mwenyewe. She is nice, very sweet Wema haingii. Ni mtu wa kujipraudi.

“Sasa chanzo cha kugombana naye, nilimpigia simu. Mambo? Clouds wamenipigia like wanataka kunipa kipindi akaniambia poa, nilipofika pale akanizuia nisiongee na mtu yeyote.

“Sasa mimi nikashindwa kujizuia, nikawa naongea na kina Soud alipogundua awaakambia wasiongee na mimi n ahata Soud aliniambia una nini na Diva mbona anasema tusiongee na wewe?” alisema Gigy.

Gigy anasema kuanzia hapo alishindwa kuelewa ni kwa nini anakuwa mtu wa hivyo na ndio toka hapo wakawa hawaivi na ilifika mahali akalazimika kuacha kazi Clouds kwa sababu ya Diva ili tu awe na amani ya moyo maana alikuwa akimkera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live