Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gigy agoma kumzungumzia Harmonize

Gigy Moneyy Gigy agoma kumzungumzia Harmonize

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo anayefanya poa kunako mitandao ya kijamii na Bongo Fleva, Gift Stanford 'Gigy Money' amesema hawezi kumzungumzia Harmonize kuhusu kutembelea nyota ya Mbosso katika kutoa albamu.

Gigy alitoa kauli hiyo Oktoba 27, 2022 alipokuwa kwenye uzinduzi wa albamu ya Mbosso ambapo mtangazaji alimuuliza juu ya mtazamo wake,kuhusu Harmonize kutoa albamu yake siku moja baada ya Mbosso.

"Mimi sitaki kujua kuhusu hilo kwanza nilikuwa sijui kama anatoa albamu lakini hayo ni yao, mimi niachojua hapa nimekuja kwa Mbosso na hata yeye akinialika basi nitaenda," alisema Gigy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live