Menu ›
Burudani
Fri, 31 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford 'Gigy Money' amekiri kuwa, hapendi kuachana na mwanaume kwa ugomvi na anapokuwa amekupenda basi anaweza kuwapenda wanaume hata watatu kwa wakati mmoja.
Gigy amesema inawezekana isiwe kimapenzi lakini anajikuta tu anawapenda wanaume hata watatu.
"Eeeh inabidi tu wanivumilie mimi ndio nipo hivyo," alisema Gigy.
Gigy amesema, suala hilo limemgharimu kwani kuna mwanaume mmoja aliwahi kuwa naye kwenye mahusiano na akazoeana sana na mwanaye.
Amesema Ex wake huyo aitwaye Crey bado yupo moyoni mwake kutokana na namna ambavyo mtoto wake Mayra amemzoea yeye kama Baba!
Chanzo: www.tanzaniaweb.live