Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gigy Money amkingia kufua Uwoya ishu ya uchungaji

Gigy Uchungungaji Wa Uwoya Gigy Money amkingia kufua Uwoya ishu ya uchungaji

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford 'Gigy Money' amesema anamuona Irene Uwoya ana kitu Mungu anataka kumtumia kupitia uchungaji.

Gigy amesema ana asilimia nyingi ya kuamini kwamba Irene ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kupitia uigizaji, habahatishi kwenye suala hilo ambalo analiishi kwa sasa.

"Mimi nina asilimia 95% Irene Uwoya kaitwa na Mungu kuwa Mchungaji, na huu mchakato hajauanza leo. Nakumbuka kuna siku nilikuwa Club nimelewa mbwiii nimepanda juu ya meza nacheza kama kawaida yangu, Irene alinipigia simu akaniambia Gigy nataka tuonane lakini naomba uje hotelini sitaki kuja Club"

"Ulikuwa ni usiku sana lakini nilimfata Irene mpaka hotelini, nilipofika akaniambia Gigy Mungu anakuita, aliniambia huku anataka kulia. Nilishangaa nikasema Irene huyuhuyu??? Kiukweli aliniambia maneno ambayo yalinibadilisha sana hiyo siku mpaka leo nakumbukaga. Kwahiyo Irene hajaanza leo kuzungumza na Mungu mimi naona Mungu ana kusudi nae kubwa"- Gigy Money, Msanii wa muziki wa Bongo Flava.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live