Menu ›
Burudani
Mon, 5 Sep 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Warembo wasioishiwa vituko, Gigy Money na Masha Love, wamesema hawawezi kusafiri peke yao kwa kipindi hiki cha baridi.
Masha Love na Gigy wamefunguka hayo wakiwa kwenye basi kuelekea jijini Mwanza ambapo walipopewa mic, kila mmoja alisema yupo na mpenzi wake kwani kuna baridi.
“Nisafiri peke yangu mpenzi wangu nimuachie nani?” alihoji Gigy ambaye alikuwa amekaa siti moja na mpenzi wake ambaye hakuonekana kuzungumza kitu.
Masha naye ambaye alikuwa amekaa siti moja na mpenzi wake ambaye hakumtaja jina, naye alisema hivyo hivyo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live