Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gigy Money:Mafanikio hayaji kwa kulazimisha kuishi kama wengine

87493 Gigypiv Gigy Money:Mafanikio hayaji kwa kulazimisha kuishi kama wengine

Sat, 7 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwimbaji Gigy Money amewashangaa wasanii wanaowaogopa wakongwe kwenye sanaa badala ya kupambana kuwafikia.

“Unatakiwa uwatizame kwa matamanio waliyofanikiwa na kuiga mazuri yao, lakini usilazimishe kupita njia zao, ukifanya hivyo matokeo ni mawili kufanikiwa au kukwama, muhimu upite njia zako unazoziamini”.

Gigy Money ambaye jina lake halisi anaitwa Gift Stanford aliliambia gazeti hili kuwa hajawahi kumuogopa mtu wala watu anapojaribu jambo lake na ndiyo maana anafanikiwa.

Alisema alianza kazi ya kuwa video Vixen kwa sababu alikuwa anataka kutafuta nafasi ya kutoka kisanii na alipofanikiwa sasa anapiga fedha kwa shoo na ubalozi wa bidhaa.

Alifafanua kuwa amefanya vitu vingi na amekutana na mambo mengi, lakini kuna kitu alikuwa anakitafuta.

“Sijawahi, sifikirii na wala sijawahi kumuogopa aliyefanya vizuri au kutangulia, ninawasifu wanawake waliofanikiwa, lakini ninawasisitiza kupita kwenye njia zao, kama mimi nimefika hapa nilipo kwa kupita kwenye njia zangu.

“Ninafanya hivyo kwa sababu kila mmoja ana njia zake za kutoka, tunaambiwa tujifunze tuige watu, unaweza kuwaiga wee! Kama siyo njia yako utaishia kutaabika tu,” alisema.

Gigy alisema kuwa pamoja na kuishi kistaa unapaswa kuwa na misimamo itakayowashawishi wengine kuona umuhimu wako.

“Unaweza kusema Gigy hana adabu, lakini huwezi kusema Gigy hana akili kwa sababu ninapopiga dili na ni mama Myra, hivyo ninatambua jukumu lililo mbele yangu la kuhakikisha mtoto wangu anapata mahitaji muhimu.

“Vyote hivyo nimevipata kupitia sanaa na katika tasnia hiyo nimeingia ili nitimize haya ninayoyafanya sasa, bado napambana na karibu nitaachia EP yangu ninaifanyia kazi kwa sasa,” alisema Gigy.

Chanzo: mwananchi.co.tz