Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gigy: Kujichetua kwangu kunanipa madili mengi

GIGY 660x400 1.jpeg Gigy: Kujichetua kwangu kunanipa madili mengi

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMAMA mtata kunako Bongo Flevani, Gift Stanford almaarufu Gigy Money, anasema kuwa, asilimia kubwa ya watu wanaokesha kumsema vibaya mitandaoni kuwa anapenda kujichetua, hawayajui maisha.

Akichezesha taya, mwanamama huyo anaeleza kwamba, maisha ni fumbo zito mno na kila mtu ana lake hivyo hao wanaosema anajichetua mitandaoni, waache waendelee kuongea kwa sababu kujichetua kwake ndiyo kunamfanya yeye na familia yake waweze kuingiza tonge mdomoni.

Kuna watu wanakaa kusema wenzao utadhani wao ni malaika, kwamba hawana kasoro hata moja, wengi wanaonisema vibaya mitandaoni bado hawajajua nini maana ya maisha, kuna muda huwa najichetua mitandaoni ili kujipa tu furaha ambayo nimeoikosa kwa watu ninaowategemea.

Lakini kujichetua kwangu pia kunanipa madili mengi ya pesa ambayo yananisaidia mimi na mwanangu,” anasema Gigy ambaye ni mama wa mtoto mmoja; juzikati alitwaa tuzo ya maeksi wanaocharuana mitandaoni kati yake na mzazi mwenzake, Mo J.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live