Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghetto Kids wapoteza katika fainali ya Britain's Got Talent

Ghetto Kids Ghetto Kids

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikundi cha densi cha Uganda Ghetto Kids kilikosa nafasi tatu za juu katika hatua ya mwisho ya shindano la Britain’s Got Talent siku ya Jumapili, na kuwashukuru mashabiki kwa "kuwaunga mkono wakati wote wa shindano hilo".

Kundi hilo la watoto sita wana umri wa kati ya miaka sita na 13, na walitoka katika jamii masikini katika mji mkuu wa Uganda Kampala kabla ya kuchukuliwa na kulelewa na mlezi wao aliyegeuka meneja Dauda Kavuma.

Ghetto Kids ilikuwa miongoni mwa waliofika fainali 10 katika shindano hilo ambalo mshindi ni Viggo Venn, mcheshi mwenye umri wa miaka 33 kutoka Norway. Nafasi ya pili ilichukuliwa na mchezaji densi Lilliana Clifton mwenye umri wa miaka 13 huku mwana mazingaombwe Cillian O’Connor, 14, akiibuka wa tatu.

Kundi hilo la Uganda tayari limeweka historia baada ya kupewa "golden buzzer" na mmoja wa majaji kabla hata hawajamaliza onesho lao, jambo lililowapeleka moja kwa moja nusu fainali. Kisha walipata kura nyingi zaidi za watazamaji, na kuwapa nafasi kwenye fainali pamoja na washiriki wengine tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live