Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gharama za maziko mwili wa Mzee wa Mjegeje zaibua mapya

Mzee Mjegeje Gharama za maziko mwili wa Mzee wa Mjegeje zaibua mapya

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thabiti Ally Kipwasa ‘Real Jimmy’ ambaye ni Meneja wa aliyekuwa msanii wa Bongo, Mzee Omar maarufu kama Mzee wa Mjegeje amefunguka kwa vile wameshindwa kushirikiana na ndugu wa marehemu, hivyo wanaomba mtu yeyote aliyeguswa na msiba huo achangie chochote ili mwili wa marehemu uweze kupumzishwa.

Thabiti ameongeza kuwa, Mzee wa Mjegeje alitoa kauli kuwa akifa asizikwe nyumbani kwao Bagamoyo, badala yake azikwe Dar es Salaam kwa sababu ndugu zake wote walimkataa wakati akiugua.

“Kwa sababu ndugu zake hawataki kukaa na sisi, kuongea na sisi vizuri, wala kuelewana na sisi na wala hawana umoja na sisi, wanakuja kiubabe hawana ubinadamu, na sisi tutaenda nao kibabe. Kama mzee leo hatoki basi inshallah atazikwa hata kesho.

“Gharama zote za kutoa mwili na mambo mengine mpaka kumpumzisha mzee wetu ni kama Tsh laki saba hivi. Yeyote yule ambaye ameguswa na hili anaweza kutuchangia chochote tumpumzishe salama kwa Amani.

“Mpaka sasa hivi hakijapatikana chochote, ndiyo tunataka tukae kiko na Aunt Lulu na Mama yangu Mama Kipwasa ili tujadili tuone tunafanya nini. Tangu akiwa hai alisema hana ndugu kwa sababu wao walimkana,” amesema Thabiti.

Mzee wa Mjegeje aliyetamba kwenye mitandao ya kijamii kwa video yake ya 'Kata simu tupo site' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 20, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matoiabu.

Mzee wa Mjegeje alikuwa msanii kutoka Bagamoyo, Tanzania ambaye alikuwa akijihusisha na shughuli zote za sanaa hasa za maigizo ya vichekesho na uimbaji wa muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live