Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Genevieve Nnaji ameugua akili?

Ganevieve Nnaji.jpeg Genevieve Nnaji

Sat, 14 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke kinara wa Nollywood, Genevieve Nnaji amekanusha uvumi unaoendelea kuwa amelazwa katika hospitali nchini Marekani kwa tatizo la ugonjwa wa akili.

Mkali huyo wa ‘Lionheart’ alichapisha video akichora picha kuonyesha hali yake ya kiakili ni sawa na mtu yeyote mwenye utambuzi wa kutosha na wenye akili timamu.

Uvumi huo ulienea baada ya kitendo cha mwigizaji huyo wa filamu kufuta machapisho yote kwenye ukurasa wake wa Instagram huku pia aki-unfollow kila mtu kwenye ukurasa wake.

Ingawa uvumi wa ugonjwa wa akili unaweza kuwa sio kweli kabisa inaonekana kuna kitu kuhusu mwigizaji huyo.

Rafiki yake wa karibu na mwanablogu, Stella Dimokokorkus alithibitisha katika chapisho la Instagram kwamba mwigizaji huyo kweli anapambana na hali yake ya tatizo la kiakili.

Kulingana na rafiki yake alichapisha kuwa; "Nimekuwa nikifahamu hali ya kiafya ambayo anapitia lakini niliamua kuiacha iendelee hadi atakapopata nafuu"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live