Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Gari la Kifahari la Mwanamfalme lazua taharuki

Gugati Divo Sheikh Joaan bin Hamad bin Khalifa Al Thani

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja wa Wana wa Mfalme kutokea Qatar, Sheikh Joaan bin Hamad bin Khalifa Al Thani amewaacha watazamaji na wenye shauku ya magari wakishangaa baada ya kuonekana kwenye mitaa ya Monte Carlo huko Monaco, Ufaransa akiwa kwenye gari ya nadra sana na yenye thamani kubwa aina ya Bugatti Divo.

Hii sio Bugatti Divo pekee inayomilikiwa na wanafamilia hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu Sheikh Khalifa bin Hamad bin Khalifa Al Thani alionekana katika mitaa ya jiji la London akiendesha gari inayotaka kufanana kabisa na hiyo ambayo imetengenezwa kulingana na Chiron.

Gari za aina hii zimetengenezwa 40 tu na zote ziliuzwa kwa wateja kabla kampuni husika kuanza kuzionyesha kwa umma.

Bugatti Divo ya bei ya chini zaidi ilikuwa ni dola za kimarekani milioni 5 huku mengine yakizidi bei kutokana na kuongezewa vipengele kulingana na mahitaji ya wateja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live