Mtangazaji wa redio mwenye sauti iliyomvutia kila mtu. Msanii wa sauti (the voice-over artist), aliyenakshi jingles. Mwendesha shughuli (MC), mwenye sanaa kubwa.
Gardner Gabriel Habash. Tangu Mzee wa Kujinafasi hadi Babu Vipensi. Kutokea Gardner G mpaka Babu G. Mtangazaji wa dansi katika Afrika Bambataa, kisha akawa haiba ya Bongo Flava, kabla ya kugeuka Captain wa drive-time shows. Gardner, the versatile.
Jahazi la Clouds FM, halafu Maskani ya Times FM, ikafuata Ubaoni EFM, kisha tena Jahazi Clouds FM. Gardner kwenye microphone, sauti ikichakatwa na mixer. Transmitter ikimsafirisha hadi ulipo. Kwa ubunifu na utundu wa kucheza na maneno. Gardner, hakuna aliyesogea anga zake.
Gardner ni role model wa vijana waingiza sauti za matangazo. Sauti na swagger za Gardner kwenye utangazaji, vimo ndani ya watangazaji wengi. Gardner ni nembo ya utangazaji wa kisasa Tanzania. Gardner ni mwanamageuzi, pia mwanamapinduzi wa tasnia ya habari Tanzania.
Unazijua habari za Midas? Ni mfalme wa Phrygia, Ugiriki ya Kale. Midas alikuwa na karama ya ajabu, kila alichoshika, alipotaka, aliweza kukibadili kuwa dhahabu.
Gardner, the Midas, kila kipindi alichokifanya kiligeuka dhahabu. Hii ilitafsiri nguvu na nyota yake. Afrika Bambataa kwenye dansi, vipindi vya Bongo Flava Clouds FM, na ule u-Captain aliojitengenezea katika shows za jioni.
Gardner, the music executive. Katika maisha yake amesimamia wanamuziki wengi ambao walipata mafanikio makubwa. Gardner, the music contributor. Maneno yake yalitumika kunogesha nyimbo nyingi za Swahili Rap na Bongo Flava.
Miaka ya 1990, Bongo Flava haikuwa mainstream music. Mageuzi makubwa yalifanyika early 2000, kuipeleka Bongo Flava mainstream. Gardner alikuwa major player, kama mtangazaji na music executive, akitoa mchango mkubwa kuifikisha Bongo Flava kwenye mainstream.
Gardner, aina yake ya utangazaji wenye swagger za kiburudani, ulifanya taarifa alizotoa zipenye na kufika kwa urahisi. Kama taarifa na burudani ni infotainment. Gardner ndiye infotainer.
Alisema Steve Jobs: “Kifo ni hatima ambayo wote tunaichangia.” Gardner ametangulia. Tuliobaki, muda wetu waja. Ndimi Luqman MALOTO