Babu Inspector Haroun na Luteni Kalama, let me raise hell kuhusu umilionea wa Gangwe Mob.
Msimu wa kiangazi unaisha mwaka 2001, Gangwe wapo top kwenye line-up ya Bongo Flava. Walipokea mkwanja mrefu zaidi kwa show. Na ziara zilikuwa nyingi.
Albamu “Simulizi za Ufasaha” imekamilika. Mauzo ya muziki yalikuwa kwa audio cassette. Wasambazaji wakubwa ni watatu; GMC, Wananchi Store na FM.
Gangwe walifika bei Sh30 milioni kwa Mamu (GMC). Enzi hizo dola moja ya Marekani ilikuwa Sh925. Hivyo, Sh30 milioni ilikuwa sawa na dola 33,000.
Kwa mujibu wa kikotoo cha mfumuko wa bei cha Benki Kuu Marekani (The Fed), dola 100 ya mwaka 2001 ni sawa na dola 172.61 mwaka 2023. Inflation rate ya dola ni asilimia 2.51 kila mwaka.
Dola 33,000 ambazo Gangwe walikubaliana na Mamu (GMC), kuuza albamu ya Simulizi za Ufasaha mwaka 2001, kwa mwaka huu (2023), zingekuwa dola 56,852.61, ambazo chenji yake ni Sh143 milioni.
Story ipo hivi; siku Gangwe (Inspector na Luteni), walipokwenda kusaini deal na Mamu, Kariakoo, walilipwa advance Sh12 milioni (dola 13,000).
Dola 13,000 mwaka 2001 ni dola 22,439.20 mwaka 2023, ambazo ukizipitisha bureau de change leo, utapata Sh56.4 milioni.
Pesa zote hizo, tena walilipwa cash, wangebebaje? Wangetoka nazo vipi Kariakoo salama? Kwa wizi na ujambazi ule!
Tupac wa Mikoroshini (Inspector), akamaliza kesi. Akaingia shimoni Kariakoo. Akanunua kikapu kikubwa, akafanya shopping ya mchicha mwingi na kabichi za kutosha. Inspector aliporejea kwa Mamu, akasema leteni hizo hela. Akapanga mchicha chini kwenye kapu. Pesa katikati. Juu kabichi.
Inspector na Luteni walibeba kapu kama wametoka kununua mboga. Wakakatiza kwa miguu hadi Mkwepu, Posta. Wakakutana na Mkurugenzi wa Gangwe, Sebastian Maganga, akawasaidia kufungua akaunti benki.
Ni history, Bongo Flava ilivyobadili maisha ya vijana. Ni excitement, Agosti 25, 2023, machampion wa Uswazi, Gangwe Mob, wataheshimishwa kupitia Bongo Flava Honors.
Gangwe Mob ni cornerstone to the contemporary Bongo Flava. Wamefanya makubwa, wanastahili heshima kubwa. Maneno yote ni Alliance Francaise.
Na Luqman MALOTO